Chumba cha Paula wa P- Funk Kufuru!


Chumba cha Paula wa P- Funk Kufuru!
  • Chumba cha Paula wa P- Funk Kufuru! 1
  • Chumba cha Paula wa P- Funk Kufuru! 2

Chumba cha mtoto wa prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P- Funk’ na Kajala Msanja, Paula kimeibua mshituko kufuatia namna kilivyosheheni vitu vya thamani.
Juzikati mwandishi wetu alitinga ndani ya mjengo anaoishi Kajala maeneo ya Mwenge jijini Dar na kustaajabu mengi lakini miongoni mwayo ni chumba ambacho ametengewa Paula.
Chumba hicho kina kitanda cha gharama, kimerembwa kwa kuandikwa jina la Paula ukutani, kuna kabati kubwa la nguo na shelfu iliyosheheni viatu kibao vya kila aina.
Hata hivyo, ikabainika kuwa, kufuru zilizomo chumbani kwa binti huyo anayesoma zinatokana na mama yake ambaye pesa inaonekana kuwa siyo shida kwa muda huu.