‘Men In Black’ bila Will Smith itakuaje, ni kweli Will Smith hatoigiza kwenye Men In Black 4!?










Kama vile ilivyo brand ya movie ya Bad Boys, movie za Men In Black haziwezi kuongelewa
bila kumtaja staa wake Will Smith na kama ulikuwa hujui basi taarifa ikufikie kuwa 
part 4 ya movie hiyo iko njiani mtu wangu lakini bad news ni kwamba Will Smithhatokuepo

kwenye movie hiyo safari hii, kwa nini!? iko hivi…




Will Smith na Tommy Lee Jones kwenye movie ya Men In Black 3 mwaka 2012.


Watengenezaji wa movie hiyo Walter Parkes na mwenzake Laurie MacDonald walipata
kueleza kwanini wameamua kutokumuweka Will Smith kwenye movie hiyo safari hii..


>>> “Tunatengeneza kama series ya muendelezo wa movie iliyopita, tutaibadilisha 
kidogo na pengine Will Smith hatoonekana kwenye muendelezo wa movie ya safari hii…
 tuna mtazamo tofauti safari hii wa jinsi tunavyotaka kuipeleka brand ya Men In Black,
 Will Smith amefanya kazi nzuri sana kwa movie zilizopita ila safari hii tumesukumwa
kufanya vitu tofauti kidogo…” <<< @Laurie MacDonald.




Walter Parkes na mwenzake Laurie MacDonald watayarishaji wa movie za Men In Black.


Movie za Men In Black zimemuingizia Will Smith hela ndefu sana kwa miaka yote aliyokuwa
 anazicheza na licha ya yeye kutokuepo kwenye movie hiyo time hii, mwigizaji huyo
 ameungana na rapper Jay Z na pamoja wanategemea kutengeneza mini series itakayo
 onyeshwa HBO hivi karibuni.





Will Smith & Jay Z.


Will Smith na kampuni yake ya Overbrook Entertainment pia wana mpango wa kutengeneza
 movie itakayofana na series ya ‘The Fresh Prince of Bel-Air’, series iliyompatia umaarufu 
mkubwa sana Will Smith miaka ya 90.