Wasanii mbalimbali wa filamu waliomo kwenye Kampeni za CCM kupitia mpango wa Mama Ongea na Mwanao akiwemo Wema Sepetu, juzikati walimliza mama wa msanii marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’ pale walipokwenda kutembelea kaburi lake.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vfQo1xW95_bVGg1y0pXaiB-yeZhMLfj6QY4lISYBtLqh9TCRSi4PYLEEU12-r-YNUhsquCcOL5WuJfsAZWWXQkBmO4iT4KuBNUZHOE-umwaY9DDeDQQS5NzobM7SMacm5TM07szXD7FJ7cKrWEsdP1Oc7rCtf5BQYSA3R1mYRWcO7r7nNpAkQwv5n-Uu-aUxWecclI0sIWp8tk8eKI2S9ryXfOA53PyIimf8QjDk5GYHN-uABL1Xz5cvA1lZ0l_1RQ7a5loFSI_A=s0-d)
“Tulipofika pale tulionana na mama Sharo, tukapiga naye stori mbili tatu lakini tuliona tusiishie pale, tupelekwe kwenye kaburi la mwanaye, hapo ndipo alipoanza kubadilika na kuonesha hali ya majonzi kisha akaanza kulia!
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vxHnqPhxTNtfNMTZ9Lh3JX_5CrUjCWxKU15nGReDcYjlVNXxsoOjdEJOowsaw3NyRv2clYqgpbn_2fS2Zj5f86wc5FElQb4fpwkEEAGEehTlMAykakDI6_IeYq67Wgcbk1k5pLjYXRzwP9QYWo7qTTp0QAUluby8P-hr3n8R0mH3Zr59c6JP39yN-rpD2j-iQz7KCBxtE2p1azoz6DSLCA5-2q4qhNJ_IuRGunl0sewDlvyx5EejTFju3pdMTWDzjmehKute5h=s0-d)
Mama wa msanii wa marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’ akilia.
Wasanii hao walichukua uamuzi huo walipopita katika kijiji alichozaliwa msanii huyo cha Lusanga, wilayani Muheza mkoani Tanga na kwenda kumsalimia mama wa marehemu lakini ilidaiwa kuwa Wema alimliza mama huyo baada ya kuonekana akilia sana bila kunyamaza.
Wema akiwa mwenye hudhuni kubwa.
“Hali ile ilitufanya wote tuliokuwa pale kupatwa na huzuni na kwa kweli wengi tulishindwa kujizuia kulia, hata tulipofika kaburini, simanzi iliongezeka lakini tukaomba dua na kuondoka,” alisema Halima Yahaya ‘Davina’ aliyekuwa mmoja wa wasanii waliokuwa kwenye msafara huo.