Ben Pol.KATIKA ulimwengu wa muziki Bongo, tumekuwa tukiwasikia wasanii wachache wakivuma ndani na nje ya nchi huku wakifanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchi tofauti na Tanzania.
Kwenye makala haya tunakuletea orodha ya mastaa wanaofanya vizuri lakini tatizo ni nyota kwani kazi zao ni nzuri lakini hawaoneshi kuwa gumzo na kupata tuzo za kitaifa na kimataifa kama walivyo hao wengine wachache.
Bernad Paul ndilo jina alilopewa na wazazi wake. Huyu ni mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva na nyimbo nyingi anazoimba na uimbaji wake ni mzuri lakini imekuwa ni vigumu kutoboa kimataifa pia kwa Bongo tuzo nazo zimekuwa zikimpitia mbali. Ben Pol ametamba na ngoma kali kama Jikubali, Unanichora, Sophia na nyingine nyingi.
Wimbo wa Masogange ndiyo uliomtambulisha kwenye anga la muziki. Abednego Damian ‘Belle 9’ aliutendea haki wimbo huo na nyingine alizowahi kuimba kama Shauri Zao, Listen na nyinginezo lakini ameshindwa kutoboa kimataifa kama walivyo akina Ali Kiba na Diamond wakati ni mwanamuziki mzuri.
Mo Music nyota yake imeshindwa kung’aa labda kutokana na kwamba hajaingia moja kwa moja kwenye muziki au la kwani alikuwa masomoni huku akiimba.
Mwanamuziki huyu hajawahi kufanya kolabo na msanii wa nje ya Bongo na amewahi kusema kwamba hana mpango wa kufanya kazi na wasanii wa kimataifa kwa sababu anaamini atatoka mwenyewe.
Barnaba amefanya vizuri kwa nyimbo zake kama Suna, Siri aliofanya na Vannesa Mdee, Wahalade ambayo ilipendwa sana na mashabiki wengi na nyingine nyingi ambapo ameshindwa kufika levo za Diamond wakati anastahili hata kumpita.