Mauaji mengine ya wanafunzi wakiwa chuoni Marekani, maneno ya Obama pia yapo hapa..(Pichaz&Video)


Marekani imekuwa ikiingia kwenye headlines mara kwa mara kuhusiana na matukio ya watu kupigwa risasi..Headlines zimerudi tena huko, ni kuhusu kijana mmoja kuvamia chuo cha Umpgua community na kuua wanafunzi 10 huku wengine saba wakijeruhiwa.

Polisi walipata taarifa hiyo baada ya mtuhumiwa huyo kufanya tukio hilo na kufika eneo la tukio..pia polisi walifanikiwa kumuua Harper Mercer ambaye anatuhumiwa kufanya mauaji hayo kwa kumpiga risasi akiwa bado eneo la tukio.
shoot
Mmoja wa mashuhuda ambaye alikua baba wa mmoja wa wanafunzi waliojeruhiwa alisema alisema kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Harper Mercer kabla ya kufanya mauaji alikua akiwauliza watu hao wanatoka dini gani kisha kuwafyatulia risasi.
shoot2
Polisi bado wanaendelea na uchunguzi kujua muuaji huyo alikua na lengo gani na kutafuta nyumba aliyokuwa akiishi.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema matukio ya watu kuua raia yamekuwa yakawaida sana na kuvitaka vyombo husika kuweka sheria ya udhibiti wa silaha za moto.
shoot3

shoot4
Harper Mercer mwenye miaka 26, kijana anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo
Obama akizungumza baada ya tukio hilo…