HIVI NDIVYO YUSUPH MLELA ANAVYOJIACHIA NA SHOMBESHOMBE ZENJI



Staa wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela akiwa na shombeshombe huyo.Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela juzikati alinaswa Zanzibar akijiachia kimahaba na mrembo shombeshombe.Chanzo makini kililitonya gazeti hili kuwa, Mlela ameonekana visiwani humo kwa wiki nzima akijiachia na mwanadada huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja bila kuhofia wala kuogopa macho ya watu.

Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusiana na hilo, Mlela alisema: “Ni kweli niko Zanzibar nimekuja kupumzika baada ya kutoka kwenye kazi Kenya, kuhusu huyo shombeshombe unayemsema mbona ni rafiki tu jamani?”