Upelelezi ukiwa bado unaendelea kufuatia ufisadi wa kupitishwa kwa
makontena takribani 350 bandarini bila kulipia ushuru. Leo jeshi la
polisi limewakamata wafanyakazi wa TRA ambao ndio wanahusika na
upitishaji wa makontena pale bandarini. Taarifa za awali zinasema idadi
ya wafanyakazi hao walioswekwa ndani inakadiriwa kuwa ni 27.