TCRA YAVIFUNGIA VITUO 27 VYA RADIO NA TV KWA KUKWEPA KODI.......MIONGONI MWA VITUO VILIVYOFUNGIWA NI STAR TV, RADIO FREE AFRICA , KISS FM,KIFIMBO FM NA IMPACT FM ZA DODOMA
Na Nasri Bakari
HAPANDAE HABA ATAVUNA HABA huo ndio usemi wa kiswahili unaoweza kutumika baada ya Mamlaka ya Mawasiliano TCRA kuvifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya TV kikiwemo kituo cha Star TV, Radio free Afrika, Kiss Fm , Uhuru FM,Impact fm na Kifimbo Fm kwa kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati ..
Akitangaza uamuzi huo, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy, amesema kuwa mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo kesho saa 6 usiku, na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili.
Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi kusema ni kiasi gani cha pesa ambacho vituo hivyo vinadaiwa kwa madai kuwa kanuni na taratibu haziwaruhusu kutaja kiasi hicho kwa kuwa ni siri kati ya TCRA na mteja.
Aidha Mungy amesema kuwa TCRA imewataka wadau wote wa mawasiliano nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata taratibu, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo la kuwasaka wanaokwepa kodi ni endelevu.
VITUO VINGINE VILIVYOKUMBWA NA MASWAHIBU HAYO NI
1. Sibuka FM
2. Breez FM
3. Country FM
4. Ebony FM
5. Hot FM
6. Iringa Municipal TV
7. Kiss FM
8. Kitulo FM
9. Mbeya City Municipal TV
10. Radio 5
11. Radio Free Afrika (RFA)
12. Musa Television Network
13. Pride FM radio
14. Radio Huruma
15. Radio Uhuru
16. Star TV
17. Rock FM Radio
18. Standard FM radio
19. Sumbawanga Municipal TV
20. Tanga City TV
21. Top Radio FM limited
22. Ulanga FM
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU
LIKE PAGE YETU YA FB HAPA