VUGUVUGU la kisiasa limekuwa kubwa katika jamii yetu kiasi kwamba kila mmoja anazungumza kuhusu siasa, hasa upinzani mkubwa uliopo hivi sasa kati ya vyama vinavyounda Ukawa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kila mmoja anaonesha jinsi gani siasa inavyomhusu na anavutia upande wake kwa nguvu zake zote. Bahati mbaya hata hivyo, wapo baadhi ya wenzetu ambao wameamua kuwapa wenzao uadui, kwa sababu tu wana mtazamo tofauti na wao.
Hili ni kosa kwa sababu katika siasa, hatuwezi kufanana, lazima tutofautiane na ndiyo maana halisi ya vyama vingi.
Hata hivyo, kuna mdada mmoja ni vizuri nikamzungumzia kwa namna ya kumshauri juu ya kitu hiki kiitwacho siasa, hasa wakati kama huu ambao nchi yetu bado haikupata kushuhudia ushabiki, upinzani na tambo baina ya vyama kama ilivyo hivi sasa.
Hata hivyo, kuna mdada mmoja ni vizuri nikamzungumzia kwa namna ya kumshauri juu ya kitu hiki kiitwacho siasa, hasa wakati kama huu ambao nchi yetu bado haikupata kushuhudia ushabiki, upinzani na tambo baina ya vyama kama ilivyo hivi sasa.
Wiki iliyopita, pale katika Jengo la Millennium Towers, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, kulikuwa na mkutano wa ndani wa akina mama wafuasi wa Chadema, tukio ambalo mgeni rasmi alikuwa mgombea urais wa vyama vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa.
Miongoni mwa makundi yaliyohudhuria tukio hilo, walikuwa ni baadhi ya wasanii wa filamu ambao walijipambanua kuwa wao wako upande huo linapokuja suala la siasa. Siku chache tu baada ya tukio hilo, CCM nao walifanya kitu kama hicho, lililopewa jina la Ongea na Mwanao, lililofanyika Hoteli ya Hyatt Regency Kempinski, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete. Kama ilivyokuwa kwa Chadema, huku nako waigizaji wa filamu walikuwepo na kutangaza ukereketwa wao.
Katika waigizaji waliotokea Millennium Tower, alikuwepo Chuchu Hans, mmoja kati ya mastaa wanaofanya vizuri katika sinema za Kibongo, akionekana akiwa katika sare pamoja na wenzake Jacqueline Wolper, Aunt Ezekiel na wengineo, kuashiria kuwa wao ni Pipooz Pawa hatari.
Lakini katika namna ya kushangaza, siku mbili baadaye, kwenye hafla ya Mama Ongea na Mwanao, Chuchu alikuwepo kuthibitisha kuwa yeye ni chama tawala wa kufa mtu.
Tendo hilo lilisababisha kutupiana maneno ya kejeli na wenzake wa Ukawa, kitu ambacho ndicho kimenifanya nijitokeze kumzungumzia. Huu ni mchezo hatari hasa kwa wakati huu.
Unaweza kufanya utani katika masuala mengine lakini siyo siasa, hasa kama hizi za kwetu ambazo tunaambiwa zimejaa matumizi makubwa ya fedha kutoka kwa wanasiasa. Watu wamewekeza na wapo katika hatua za mwisho kuona zinawasaidia kufikia malengo yao.
Ingawa mwenyewe amedai aliamua kurudi CCM baada ya kuona kule alikoenda awali hakujakidhi vigezo vyake, lakini hili haliwezi kuwazuia watu kujenga hisia kuwa huenda alipata ushawishi wa ziada kuweza kuhama vyama ndani ya saa 48.
Wenyewe wanasema siasa ni mchezo mchafu, dakika moja tu inaweza kubadili kila kitu.
Unaweza kuona kitu kidogo, lakini kuna watu wengi wamepoteza maisha yao kwa sababu ya siasa, hasa unapokuwa mtu mwenye wafuasi kama alivyo Chuchu.
Wenyewe wanasema siasa ni mchezo mchafu, dakika moja tu inaweza kubadili kila kitu.
Unaweza kuona kitu kidogo, lakini kuna watu wengi wamepoteza maisha yao kwa sababu ya siasa, hasa unapokuwa mtu mwenye wafuasi kama alivyo Chuchu.
Ni lazima mtu uwe na upande, tena unaofahamika. Afadhali mtu akakuchukia lakini ukawa na msimamo wako, kwa sababu kama nilivyosema pale mwanzo, kutofautiana katika siasa ni jambo lililo wazi. Watu wote hatuwezi kuwa Ukawa, CCM au vyama vingine.