Good news mtu wangu; wimbo wa ‘Nana’ wagonga nafasi ya juu kwenye countdown ya radio Uingereza


nana
Siku chache zilizopita nilikusogezea good news iliyokuwa inawahusu watu wetu Navy Kenzo ambao wimbo wao wa ‘Game’ waliomshirikisha Vanessa Mdee ulishika #1kwenye countdown ya radio nchini Nigeria.
Licha ya hivyo wasanii wengi wa Bongo Flava wamekuwa wakiiwakilisha Tanzania vizuri sana, wapo akina Joh Makini, Jux, Alikiba na wengine. Kwa kweli sitoacha kusema wasanii wetu wanajituma na kufanya kazi kwa bidii sana.
nana2
Good news nyingine tena inatoka Uingereza mtu wangu na inaandikwa na mtu wetuDiamond Platnumz amabaye kwenye countdown ya DNA Top 5 kwenye radio ya BBC Radio 1Xtra kipindi kinachoendeshwa na DJ Edu wimbo wa Diamond ‘Nana’aliomshirikisha Flavor kutoka Nigeria umesikika kwenye nafasi ya #1 wiki hii!
nana3
BBC Radio 1Xtra ilichukua time kupitia page yake ya Twitter kumpongeza Diamond kwa kushika nafasi hiyo wiki hii.
nana
Licha ya hayo video ya ‘Nana’ ya Diamond Platnumz iliachiwa mwezi May tarehe 29 ambayo ni miezi 3 iliyopita lakini ukitembelea page ya Youtube ya msanii huyu muda huu utagundua kuwa kwa miezi hiyo 3 tu video hiyo imepata watazamajiMillion 4,064,938  na kwa hilo well done Diamond!
Hii ndio Top 5 ya DNA Top 5 wiki hii kwenye BBC Radio 1Xtra..
  1. Diamond feat. Flavour – Nana
  2. Patoranking feat. Wande Coal – My Woman, My Everything.
  3. Wizkid feat. Drake &Skepta – Ojuelegba (Rmx)
  4. Khulichana feat. Patoranking – No Lie.
  5. Davido feat. Meek Mill – Fans Mi.