Ben Pol ambaye ni mwimbaji staa wa R’n’B ambaye ni mshindi wa tuzo za KTMA ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao hawajaonekana kwenye kampeni za kisiasa mwaka 2015 kwenye headlines za uchaguzi mkuu wakipigia debe chama chochote.
Mkali huyo alipofika TZA kwenye studio za Millard Ayo Sept 25 2015 alitaja sababu kwanini haonekani kwenye majukwaa ya kisiasa >>> ‘kusema kweli nimekuwa mzito sana kuona kama ni sawa au sio sawa yaani nimekuwa mtu ambaye niko slow sana, kuna wakati hata mtu akiniuliza Ben unafanya kampeni moyoni mwangu inanichukua muda mrefu kumjibu lakini sijapata majibu mpaka sasa mimi naangalia tu kama shabiki naona tu watu wanapost huyo mara huyo‘
Play hii sauti hapa chini ili kumsikiliza Ben Pol.