Muandaaji na muigizaji wa filamu , Jimmy Mafufu amesema hawezi kuhama Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa sababu kila upande wa siasa una changamaoto zake.
Mafufu amesema alihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenda UKAWA kwasababu matatizo mengi yanayohusiana na sanaa ya filamu yalikuwa hayajapatiwa ufumbuzi na serikali yake.
Ameseme yupo UKAWA iliyomsimamisha Edward Lowassa kuwa mgombea Urais wake katika uchaguzi wa mkuu mwezi ujao kwasababu anaamini atafikia malengo aliyojiwekea akishinda kiti hicho.