Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea jana ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Alisema pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
Alisema ataongeza zaidi kasi yake katika utendaji tofauti na alipokuwa Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa akichaguliwa na watanzania kuwa rais yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
Dr John Pombe Magufuli pia alitembelea na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumbani kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu John Damiano Komba katika kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni Mjumba wa Kamti kuu ya CCM Ndugu William Lukuvi.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John Komba huko Lituhi mkoani Ruvuma.
Umati uliohudhuria katika mkutano huo
Mwigulu Nchema akitema cheche kwenye uwanja wa majimaji