Nisha Asusiwa Bethidei


Nisha Asusiwa Bethidei
     

    NI sheedah! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya mastaa wenzake kususia shughuli ya siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’.
    Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita katika Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi-Beach, Dar lakini cha ajabu hakuna staa hata mmoja aliyehudhuria zaidi ya timu yake ‘Team Nisha’ na muongozaji wake wa filamu, Leah Richard ‘Lamata’.
    Kutokana na kitendo hicho, Nisha alihuzunishwa na kitendo hicho kwani hakutegemea kama wangemfanyia hivyo kwa kuwa walikuwa na mwaliko.
    “Lakini yote kwa yote namshukuru Mungu kwa kuwa nimetimiza miaka kadhaa,” alisema Nisha aliyejikuta akiangua kilio cha furaha wakati akikata keki.