Matt Mooney ni Engineer wa Dallas Marekani, anasema hiki alichokifanya ni moja ya ndoto ambazo aliwahi kuziota tangu akiwa mdogo.. huku kwetu tumezoea makontena yale ambayo yanabeba mizigo kwenye meli na magari makubwa, watu wengine huwa wanayatengeneza na kuyafanya maduka, au vibanda vya biashara nyingine tu.
Nimevutiwa na huu ubunifu kiukweli.. jamaa kachukua kontena zake kama 14 hivi, katengeneza mjengo.. yani ukiziona hizo pichaz za ndani unaweza hata usiamini kwamba huu ni mjengo ambao umekamilika kwa kutumia kontena tu !!
Hapo mwanzo kabisa, konteni linashushwa.