Ray: Wasanii Tusitumike Kama ‘Big G’


Ray: Wasanii Tusitumike Kama ‘Big G’
     

    Staa wa Bongo Movies, Vicent Kigosi amewatahadhalisha wasanii wenzake kuwa wasitumike kwenye kampeni za uchaguzi za mwaka huu bila kuangalia nani hasa atakaesaidia tasnia ya sanaa.
    Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa instagram, Ray aliandika
    Wasanii tuwe makini sana na campaign za siasa za mwaka huu tusitumike kama bigijii watutafune alafu watuteme, tuwe makini kumsapoti mgombea atakayesaidia tasnia ili maisha yetu yasogee hata kumi mbele, si kwa kudaganywa na pesa. Utabaki kuwa ni mtazamo wangu tu wasanii tamke kutetea maslahi yetu wakati ndio huu.