Mrema Atangaza Kumuunga Mkono Mgombea Urais wa CCM John Magufuli Wakati Chama Chake TLP Kina Mgombea Urais Pia
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgx9M-vG1p5vEnxRSk1zpQApgy4RDwHwPy4fkja7CqHpUiyfjyHv0yrhxXKcvo8St-gq2sVDHkKhLFOOJAmRV4OL56W317f8wQXasMQymV870OqIte7fyEnveyAYjvnu17Tht1yjAKZET0/s400/mremaz.jpg)
Magufuli alisema pia kwamba mrema akichaguliwa atamwingiza kwenye baraza lake ya mawaziri.
Wakati hayo yakijiri viwanja vya himo, Mrema alikuwa njia panda na wakati Magufuli amemaliza mkutano wake alipita na 'entourage' yake kuelekea Same.
Mrema alikuwa amesimama anaongea na watu hapo njia panda, msafara wa Magufuli ulimpita Mrema kuelekea Same, lakini baada ya dakika 10 convoy ya Magufuli ilirudi njia panda ili kumsalimia mrema, wakazi wa Vunjo walifurika na Magufuli alimwomba Mrema aongee kidogo. Mrema alimsifia Magufuli kwa barabara alizojenga katika jimbo la Vunjo.
Magufuli nae alirudia akisema mbatia hafai kuwa mbunge ila wamchague Mrema ambaye ni jembe na mchapakazi kama yeye na watu walilipuka kwa shagwe.