HAPA NA PALE: Staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewaponda baadhi ya watu ambao hupenda kuvumisha mambo hasa kupitia mtandao picha wa Instagram kuhusiana na habari zizilosambaa siku za nyuma kuwa staa huyo ana ujauzito huku picha hiyo hapo juu ikitumika kuonyesha mimba yenyewe.
“Mimba yangu hii ilianzia Insta ikaishia insta. Pale unapoamua kufanya project zako binafsi na viungo vyako.Mana watu wakufanya nao project wameisha...wote washafanya project na washafanywa project,” Lulu aliandika hayo leo kwenye ukurasa wake wa insta mara baada ya kuweka picha hiyo hapo juu.