Mwigizaji wa filamu za vichekesho,Masanja alikuwa ni mmoja kati makada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) waliochukua fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Ludewa kwa ajili ya kumrithi aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo aliyefariki kwenye ajali ya helkopta,marehemu Deo Fulikunjombe amezungumza sababu ya kushindwa kwenye amezungumzia sababu kushindwa kwenye kinyang’anyiro hicho,alipata kura 19 huku mshindi ambaye ni Deo Ngalawa akiibuka kwa kura 537.
’Cha kwanza kabisa ambacho sikutegemea nilichokuwa najua kura zitapigwa na wananchi wale wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi lakini habari ikaja ya tofauti kuwa kura hazitapigwa na wanachama za kawaida wa CCM zitapigwa na viongozi wa CCM ngazi za wilaya walitoka viongozi watano watano kutoka kwenye kila kata na matawi kwahiyo hiyo ilikuwa picha ya tofauti kwangu kwa sababu nilikuwa makombora kwa ajili ya wanachama wangu wa kawaida sasa ukifika pale unakutana na viongozi watupu hiyo ilikuwa ndivyo sivyo vile ambavyo nilikuwa nawaza,’’ Alisema Masanja. ‘’Kura hazikutosha kwahiyo najipanga kwa ajili ya mwaka 2020 nitakuwepo tena eneo la tukio kuomba tena ridhaa ya wananchi na nimejipanga vizuri vya kutosha,’’alisema Masanja