Mkulima wa Columbia aokota dolla Million 600 shambani kwake, zinadaiwa kuwa za Pablo Escobar
Mara yako ya mwisho kuokota pesa ilikua lini ? labda kama ungekuwa unaishi Columbia ila sio Tanzania , umewahi msikia muuza madawa ya kulevya maarufu Pablo Escobar aliyekuwa anatengeneza pesa ndefu hadi anazifukia? bahati ya kuziokota moja za pesa hizo imemdondokea mkulima mmoja wa Columbia.
Mkulima mmoja anayejulikana kwa jina la Jose Mariena Cartolos ameokota kiasi cha dolla million 600 za kimarekani shambani kwake, pesa hizo zimedaiwa kuwa moja ya mamilion ya muuza madawa wa nchini humo, Pablo Escobar aliyoyafukia miaka ya nyuma.
Hata hivyo mkulima huyo hatoweza kuzichukua pesa hizo, Serikali ya Columbia imesema zitatumika kwenye kazi zingine za kusaidia wananchi kama Elimu na Afya, maafisa wa nchini humo wamesema wanahofu watu wengi zaidi wataanza kuchimba ilikutafuta pesa zingine za Pablo Escobar.
Moja ya nyumba za Pablo Escobar
Pablo Escobar alikua mmoja ya wauza madawa ya kulevya wa kwanza kuingiza Cocain marekani hivyo kumfanya kuwa moja ya matajiri wakubwa duniani, utajiri wa Pablo Escobar unafika kiasi cha dolla Billion 30.