DAH! Imebuma! Lile penzi lililoziba masikio ya wengi kati ya waigizaji wakubwa Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans linadaiwa kuanguka chali kufuatia mume wa mwanamke huyo kutua nchini kimyakimya na hivyo kuwa wigo wa wawili hao kukutana kama zamani.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu zaidi na Chuchu (jina lipo), ujio wa mwanaume huyo umemfanya Chuchu kuwa mbali na Ray hivyo penzi lao kuparaganyika.
“Yaani ngoma ilikuwa nzito. Ndiyo maana siku hizi Ray na Chuchu hawako beneti. Hata kwenye bethidei ya Wema (Novemba 1, 2015), Chuchu alifika, Ray hakutokea. Unajua Chuchu hadi sasa anasubiri uamuzi wa mwanaume huyo, ninavyojua penzi lake na Ray halipo tena,” alisema rafiki huyo.
Amani lilimtafuta Chuchu kupitia simu yake ya mkononi ili kusikia kauli yake, akasema:
“Jamani, hakuna kitu kama hicho, suala la mume wangu kuwa nchini sitaki kulizungumzia wala siyo matangazo. Ni suala langu na yeye, tafadhali sana naombeni mambo hayo muachane nayo. Ni ya kifamilia zaidi.”
“Jamani, hakuna kitu kama hicho, suala la mume wangu kuwa nchini sitaki kulizungumzia wala siyo matangazo. Ni suala langu na yeye, tafadhali sana naombeni mambo hayo muachane nayo. Ni ya kifamilia zaidi.”
Amani lilimtafuta na Ray angalau kuambulia chochote, lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa. Akatumiwa meseji napo hakujibu.Kwa upande wa Johari aliyewahi kuwa mpenzi wa Ray alipotafutwa na kuelezewa juu ya hili aliishia kucheka tu.