JAPOKUWA uchaguzi umekwisha bado lile bifu la wasanii wa filamu Bongo, Jimmy Mafufu na Musa Yusuf ‘Kitale’ linaendelea kufukuta ambapo Mafufu ameapa kwamba hawezi kuzungumza na msanii huyo kwani ni mnafiki.
Akistorisha na paparazi wetu, Mafufu alisema japo mambo ya siasa za uchaguzi yameisha lakini hawezi kuzungumza na Kitale kwani ni mtoto mdogo sana kwake na ni mnafiki hivyo hawezi kushindana na mtu ambaye siyo levo yake.
“Siwezi kuongea na yule mtoto maana ni mnafiki halafu yeye ndiye anatakiwa aje aniombe msamaha maana hatulingani,” alisema Mafufu.
Mafufu na Kitale waliingia kwenye bifu baada ya kutofautiana kiitikadi za siasa ambapo Kitale alirudi CCM huku akimwacha Mafufu ambaye alimfanyia mpango wa kuonana na Lowassa. Mafufu akaona Kitale ni ndumilakuwili ndipo wakaanza kurushiana maneno makali.
Chanzo: GPL