Wema Sepetu Kanihamasisha Kuimba Muziki - Leyla






Msanii wa kike ambaye ameingia kwenye muziki wa Bongo Flava na kuachia wimbo wake mmoja wenye mahadhi ya Reggae Leyla Walden, amesema msanii Wema Sepetu ndiye aliyemuhamasisha kuingia rasmi kwenye muziki.

Leyla ameyasema hayo alipokuwa akiongea na East Africa Radio, na kueleza kuwa baada ya Wema Sepetu kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa binti huyo ana kipaji, ilikuwa ni msaada mkubwa kwake na kuamini kuwa anaweza kufanya kitu.

"Nimekuwa nikiimba muda mrefu tangia nipo mdogo, it has been my hobby, lakini kilicho insipire kutoka to the world na kuonyesha ni Wema Sepetu, she was my idol, sasa siku fulani kaniona naimba kwenye Instagram akacoment kuwa i have a gift, the fact ni Wema Sepetu na my Idol kwa kuandika tu vile ali play a very big role", alisema Leyla

Pamoja na kutoa wimbo huo ambao kwa sasa umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii, Leyla amesema kuwa hajaingia kwenye muziki kushindana na msanii yeyote, na wamchukulie kama mdogo wao.

"Sijaingia kwa ajili ya kucompete na any one, mi najua nafanya with my heart, unajua mi ninavyoimba ninafurahi, sijafanya mpaka sasa kuimba nacompete, so if it hapens nimewafikia and i hope nitafika, mimi i just wanna reach there, unajua naonekana kama kitoto fulani hivi, so kwa wote huwa napenda mi wanichukulie kama mdogo wao", alisema The Voive fairy.

Leyla pia amewataka mabinti wengine kutoogopa kufanya kile wanachopenda kwa kuhofia kutofanikiwa, kwani hata yeye alipitia huko.

"If you have a talent don't hold it in, nimekuwa napenda kuimba for the very long time sana, lakini nimekuwa nikiogopa, like sijiamini naona kama vile sijui nitafanya vipi, ideology and here i am", alisema Leyla.

Msanii huyo amesema pamoja na kutoa wimbo huo wenye mahadhi ya reggae, anafikiria kufanya muziki wenye mahadhi tofauti tofauti, na kuwataka mashabiki wake kumpa ushirikiano.

Chanzo:EATV.TV