Skip to main content
P Funk Majani kumrudisha Jay Moe
Muandaji wa muziki, P Funk Majani akikutana na Juma mchopanga au Jay Moe huwa wanaachia Hit.
P Funk ameiambia East Africa radio kuwa amefanya kazi mpya na Jay Moe ambayo itatoka hivi karibuni, tutegemee kitu kikubwa hasa ukizingatia kuwa ni muda mrefu Jay Moe hajaachia kazi mpya na umepita muda kidogo tangu studio za Bongo records kuachia kazi mpya.
Mtayarishaji na mmiliki wa studio ya ‘B Hits’ Hermy B ni mmoja ya watu waliofurahishwa na taarifa hiyo ya ujio mpya wa Jay Moe, amesema anaisubiri kwa hamu kwasababu ni moja ya combinationa anzozikubali zaidi.
Wakongwe hao wawili wana historia ya kufanya kazi pamoja na kazi zao huwa zinapokelewa vizuri.